MAYOTE FARM
Chamazi Farm |Temeke, Dar es Salaam
MAYOTE KUKU FARM ni biashara inayojihusisha na uuzaji wa vifaranga vya kuku wa kienyeji wenye afya, kwa lengo la kuwasaidia wafugaji kuanzisha na kukuza ufugaji wenye tija.
Tunazingatia upatikanaji wa vifaranga bora vinavyoweza kuwa mwanzo mzuri kwa mfugaji anayelenga uzalishaji wa kuku wa kienyeji kwa ajili ya mayai, nyama na kukuza kundi lake la mifugo.
Huduma Zetu
Uuzaji wa kuku wa kienyeji Mbegu kubwa.
Uuzaji wa vifaranga vya kuku wa kienyeji.
Kuwahudumia wafugaji wanaoanza na wale wenye uzoefu.
Kutoa maelekezo ya msingi kuhusu malezi na utunzaji wa vifaranga.
Kuhudumia oda za vifaranga kulingana na mahitaji ya mteja.
MAYOTE KUKU FARM ni chaguo kwa wafugaji wanaotafuta vifaranga vya kuku wa kienyeji na huduma inayolenga kujenga msingi mzuri wa ufugaji wao.
Sifa za MAYOTE KUKU FARM
Kuku wa kienyeji Mbegu kubwa
Kuku wanaostahimili hali yoyote ya hewa.
Kuku wazuri wa Nyama na Mayai Matamu.
Kuku wanaotamia na kulea VVifaranga wao wenyewe
Kuku wanaotaga Mayai Kuanzia miezi 4 – 5.
Vifaranga wetu wote wamepata chanjo ya awali.
Kauli Mbiu Yetu
“Vifaranga wenye Afya, Mwanzo wa Mafanikio.”
Tunaamini kuwa mafanikio katika ufugaji huanza na kuchagua vifaranga bora na kuwapa malezi na matunzo yanayofaa tangu mwanzo.
Mahali Tunapatikana
📍 Dar es Salaam — Chamazi Temeke, Tanzania
MAYOTE KUKU FARM — Vifaranga wenye Afya, Mwanzo wa Mafanikio.
Explore MAYOTE FARM's products
Browse selected products and services. Open details for more information before checkout.